NAMNA 9 ZA KUMPENDA MPENZI WAKO KWA VITENDO
Kama ilivyo mambo mengine kuwa na
ubunifu ni suala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa kwenye jamii
yenye mfumo dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo
hitaji, ebu tuliite “kupenda kwa vitendo” huenda sio kwamba hataki bali hajui.
Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe
mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa hujui
basi jifunzeni wote ili kuwa na uhusiano bora wenye furaha kwa kufuata
haya mambo machache ambayo wanawake wengi huwa hupenda kufanyiwa ili
wajue kweli wanapendwa kihisia na vitendo.
Hakuna kitu wanawake wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa busu mara kwa mara.
Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha
umemkumbatia na kumbusu hata kama kalala (hakuna raha kama kuamshwa na
busu au mkumbatio).
-
Mwambie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati, mayai, viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.
Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap
na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda
kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje
baada ya kupata kifungua kinywa.
Onesha unajali kwa kumjulia hali
kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na
vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako
pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali
unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani.
Ufikapo nyumbani mkumbatie na busu la mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.
Mnunulie vijizawadi
mara kwa mara, Wazaramo hununuliwa khanga au hereni na mikufu ya
dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti,
kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kesi;
mwanamama anafurahi kwelikweli sasa wewe fanya kile unachomudu sio kila
siku wala kila mwezi.
-
Msaidie kusafisha meza au jamvi mara baada ya mlo wa jioni,
ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani
‘mna-share’ kufanya usafi ili kuokoa muda.
Lolote litakalotokea kila la kheri, lakini hakikisha unambusu na kumkumbatia kabla hujaanza kukoroma.
No comments:
Post a Comment